Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiy ayataja mataifa ya kigeni kuingilia mazungumzo ya amani Ethiopia

Abiy Pic Abiy ayataja mataifa ya kigeni kuingilia mazungumzo ya amani Ethiopia

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema kuna "uingiliaji mkubwa wa kigeni" katika kuendelea kwa mazungumzo kati ya serikali na utawala wa Tigray lakini ana matumaini kwamba makubaliano ya amani yatafikiwa.

Akizungumza na Mtandao wa Televisheni ya Kimataifa wa China (CGTN), Bw Abiy alisema Waethiopia wanaweza kutatua masuala yao licha ya shinikizo la kimataifa la kusitisha mapigano. "Bila shaka, ikiwa kuna hatua nyingi kutoka kushoto na kulia, ni vigumu sana," Bw Abiy alisema. "Waethiopia wanapaswa kuelewa kuwa tunaweza kutatua masuala yetu sisi wenyewe."

Pia alithibitisha jeshi la serikali kukamata miji ya Tigray ya Shire, Axum na Adwa mwezi uliopita kutoka kwa waasi wa Tigray People's Liberation Front (TPLF).

"Tunajaribu kuishawishi TPLF kuheshimu sheria ya nchi, kuheshimu katiba na kuwa nchi moja nchini Ethiopia," alisema.

Wakati huo huo, msemaji wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat alisema Jumatatu "hakuna kikomo cha tarehe" kwenye mazungumzo hayo, kwa mujibu wa AFP.

Mazungumzo hayo yaliyoanza tarehe 25 Oktoba nchini Afrika Kusini yaliendelea siku ya Jumatatu ingawa yalitarajiwa kumalizika Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live