Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiy atunukiwa medali ya heshima UN

Bw Abiy Abiy atunukiwa medali ya heshima UN

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Ethiopia jana Jumapili alitunukiwa medali ya fahari ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) huko Rome Italia. Abiy Ahmed ametunukiwa nishani hiyo kutokana na maono, uongozi na kujitolea kwa serikali yake katika masuala ya usalama wa chakula na lishe pamoja na kufuatilia njia bunifu za kujitosheleza katika upatikanaji wa ngano.

Shirika la FAO limesema kuwa Medali ya Agricola inawawenzi kwa kuwatunuku nishani shakhsia mashuhuri wanaojitolea na kuunga mkono juhudi za kukuza uzalishaji endelevu wa chakula, kushughulikia suala la usalama wa chakula duniani na ushirikiano wa kimataifa.

Abiy Ahmed Waziri Mkuu wa Ethiopia alitoa shukrani zake kwa alitoa shukrani zake kwa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) kwa kumtunuku nishani ya kifahari ya Agricola kufutaia jitihada za nchi yake za kuhakikisha kuwa usalama wa chakula unadhaminiwa.

Waziri Mkuu wa Ethiopia ametunukiwa tuzo hiyo ya fahari ya FAO huku nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ikishuhudia ukame mkubwa kuwahi kuiathiri nchi hiyo katika miongo kadhaa. Ripoti zinasema kuwa watu wasiopungua milioni nne wanahitaji msaada wa dharura wa chakula huko Ethiopia. Ukame Ethiopia

Mapema mwezi huu Kamisheni ya Kushughulikia Majanga ya nchi hiyo ilieleza kuwa hali ya mambo ilizidi kuwa mbaya kutokana na viwango vya utapiamlo na uhaba mkubwa wa maji pamoja na kuongezeka kwa milipuko ya magonjwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live