Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amekutana na viongozi wa Tigray kwa mara ya kwanza tangu pande mbili zilipotia saini mkataba wa amani miezi mitatu iliopita.
Picha zilizochapishwa na vyombo vya Habari vya serikali Ethiopia vinamuonyesha Waziri mkuu Ahmed na maafisa wengine wa serikali wakiwa wamekaa na viongozi wakuu wa Tigray akiwemo kamanda wa vikosi vya Tigray Jenerali Tadesse Worede.
Wanaarifiwa kujadili hatua iliopigwa katika kutekeleza mkataba wa amani Pamoja na masuala yanayohitaji kushughulikiwa zaidi.
Makubaliano hayo yalisitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalioligubika eneo la kaskazini nchini humo.
Mkutano huo unaarifiwa kufanyika katika hoteli moja kusini mwa Ethiopia.