Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba anakusudia "kutekeleza kwa uaminifu" makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini kati ya serikali ya muungano na vikosi vya Tigraya.
Makubaliano hayo yalitiwa saini tarehe 2 Novemba ili kumaliza miaka miwili ya mapigano makali katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi.
Licha ya makubaliano hayo, vifaa vya msaada wa kibinadamu vilikuwa havijafika katika eneo hilo hadi leo, na kusababisha mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Adhanom, kutaka msaada huo uwasilishwe haraka.
Bw Ghebreyesus aliongeza kuwa watu wengi wamekuwa wakifa kutokana na magonjwa yanayotibika na njaa.
Shirika la misaada linaloongoza, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, leo limeandika kwenye Twitter kwamba msafara wao wa kwanza umefika mji mkuu wa Tigray, Mekelle, ukiwa na vifaa vya matibabu vya dharura.