Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiy Ahmed aapishwa tena kuwa Waziri Mkuu Ethiopia

TENA 1010 Abiy Ahmed aapishwa tena kuwa Waziri Mkuu Ethiopia

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameteuliwa na kuapishwa tena kushika nafasi hiyo kwa muhula wa pili kufuatia ushindi mkubwa wa chama chake katika uchaguzi Mkuu wa mwezi juni nchini humo.

Abiy alichaguliwa na Chama chake cha 'Prosperity Party ' kuwania nafasi hiyo na kisha kuteuliwa na Baraza la Wawakilishi Bungeni.

Kiongozi huyo ameapishwa mbele ya Rais wa Mahakama Kuu ya nchini humo kuwa kiongozi Mkuu wa nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri pamoja na Amri Jeshi Mkuu kwa kipindi cha miaka mitano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live