Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria wafariki katika ajali ya boti Nigeria

Abiria Wafariki Katika Ajali Ya Boti Nigeria Abiria wafariki katika ajali ya boti Nigeria

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Takriban watu watano wamefariki na wengine zaidi ya 30 kuokolewa baada ya ajali ya boti nchini Nigeria.

Boti hiyo ilipinduka siku ya Jumapili kando ya Mto Niger katika jimbo la kusini-mashariki la Anambra.

Mamlaka bado inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo, msemaji wa polisi wa jimbo hilo Tochukwu Ikenga aliambia vyombo vya habari vya ndani.

Ajali za mashua hutokea mara kwa mara nchini Nigeria, mara nyingi kutokana na matengenezo duni na mbinu dhaifu za usalama, ikiwa ni pamoja na kupakia mizigo na abiria kupita kiasi.

Chanzo: Bbc