Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria 11 Abiria ndege ya UN wanusurika kufa

D6a25802b0d5498722e750e0bfd36cf9 Abiria 11 Abiria ndege ya UN wanusurika kufa

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ABIRIA 11 wamenusurika kifo baada ya ndege ya Umoja wa Mataifa (UN) aina ya Antonov An-72 kutua kwa shida na kisha kuteleza na kwenda nje ya njia yake kwenye Uwanja wa Gao nchini Mali juzi.

Hayo yalithibitishwa na Ujumbe wa Amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSMA) ambapo askari wa UN wanasambazwa katika Jiji la Kaskazini la Gao.

“Ndege ya MINUSMA kutokea Bamako ikiwa na watu 11 ambapo wanne miongoni mwao ni wafanyakazi wa UN na saba ni wafanyakazi wa ndege, ilitua kwa shida katika Uwanja wa Ndege wa Gao,”ulisema Ujumbe wa UN na kuongeza kwamba mtu mmoja aliumia vibaya na wengine kumi walipata majeraha madogo.

Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika vituo vya kutolea huduma za afya vya kijeshi na MINUSMA kwa matibabu, huku ndege hiyo aina ya Antonov An-72 ikiwa imeharibika vibaya. Kwa mujibu wa MINUSMA, uchunguzi wa ajali hiyo utaanza mapema iwezekanavyo ili kubaini chanzo chake.

Mbali na ajali hiyo, nchini Sudan nako mazungumzo kati ya nchi hiyo, Misri na Ethiopia yalianza tena Jumatatu wiki hii kuhusu kujazwa na kuanza kazi kwa bwawa kubwa la GERD lilipo Ethiopia. Hayo yalibainishwa na Wizara ya Umwagiliaji na Rasilimali Maji ya Sudan.

“Pande hizi tatu zimekubaliana kuendelea na mazungumzo kwa ngazi ya wataalamu na kisha kufuata mazungumzo kwa ngazi ya Wizara Agosti 6 mwaka huu,”ilisema Wizara hiyo.

Waziri wa Umwagiliaji na Rasilimali Maji wa Sudan, Yasir Abbas, alisema kuwa ni muhimu kusaini makubaliano kati ya nchi hizo tatu kwa kuzingatia Bwawa la Nile. Hata hivyo, wakati wa mazungumzo hayo, Misri ilipinga uamuzi binafsi wa Ethiopia wa kuanza kulijaza bwawa hilo.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya Misri ilipinga kitendo hicho cha Ethiopia kwa sababu hakukuwa na mashauriano au makubaliano na Misri na Sudan.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Mohamed Abdel-Atti, alisema “Kitendo cha Ethiopia kuanza kujaza bwawa hili, kina maana hasi ambayo inaonesha kuwa Ethiopia haitaki kufikia makubaliano ya haki. Kitendo hiki cha Ethiopi ‘kinakiuka Azimio la Kanuni’ lililosainiwa mwaka 2015.”

Chanzo: habarileo.co.tz