Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yazitaka Kenya na Somalia kumaliza tofauti zao

Mtanzanianews 132045962 392249785371891 5618029792690029376 N 660x400 AU yazitaka Kenya na Somalia kumaliza tofauti zao

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Umoja wa Afrika unasema hatua ya Somalia, kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Kenya, unahatarisha usalama na uthabiti wa eneo la Afrika Mashariki na pembe ya Afrika.

Kauli hii imetolewa na rais wa Tume ya Umoja huo, Moussa Faki Mahamat, baada ya viongozi kutoka mataifa ya IGAD, kukutana nchini Djibouti mwishoni mwa wiki iliyopita, kujaidliana kuhusu mvutano huo.

Haya yanajiri wakati rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alikutana ana kwa ana na mwenzake wa Somlia Mohamed Abdullahi ambaye wiki iliyopita, alivunja uhusiano na Kenya kwa madai kuwa nchi hiyo inaingia siasa zake za ndani kuelekea uchgauzi Mkuu mwaka ujao, madai ambayo Kenya imekanusha.

Siku ya Jumatatu Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alikutana na kufanya mazungumzo na rais wa jimbo linalojitegemea na ambalo lilitangaza kujitawala la Somaliland, Muse Bihi Abdi.

“TUWE NAO KARIBU WANAVUNJA VIKOBA” TAZAMA WANAWAKE WAKIVUNJA KIKOBA

Chanzo: millardayo.com