Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yatoa mafunzo kwa makamanda 26 Somalia

AU SOMALIA MAKAMANDA AU yatoa mafunzo kwa makamanda 26 Somalia

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kimesema kuwa kimemaliza mafunzo ya siku 10 ya makamanda wakuu 26 wa Jeshi la Polisi la Somalia (SPF) ili kuwaongezea ujuzi na utaalamu wa kukabiliana na uhalifu na kusaidia kuimarisha hali ya usalama nchini humo.

ATMIS imesema kuwa, mafunzo ya kina kuhusu usimamizi wa kituo vya polisi yaliyofanyika katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu, yamejikita kwenye masomo ya nadharia na vitendo.

Naibu Kamishna wa Polisi wa ATMIS, Martin Amoru ameema katika taarifa iliyotolewa mjini Mogadishu kwamba makamanda wa polisi ndio kiini cha usalama wa jamii na wana nafasi kubwa na muhimu katika juhudi zinazoendelea za kuleta utulivu nchini Somalia.

Taarifa hiyo ya ATMIS aidha imesema, askari hao wakiwemo makamanda wa vituo na manaibu wao kutoka vituo mbalimbali vya polisi mjini Mogadishu, wamechukuliwa kwa kuzingatia vigezo na kutoka nyuga mbalimbali na mafunzo yaliyotolewa yamehusu sekta mbalimbali za kipolisi zikiwemo ikiwemo kanuni za maadili, uwajibikaji na uangalizi wa polisi, majukumu ya askari mkuu wa kituo cha polisi, ulinzi kwa watoto wadogo na ufanisi wa polisi jamii katika kulinda raia wakati wa mashambulizi ya kutumia silaha. Kikosi cha Kulindi Amani ya Umoja wa Afrika Somalia

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mafunzo hayo yalihusu pia mbinu za uchunguzi wa uhalifu, kukamatwa na kuwekwa kizuizini washukiwa, upelelezi, upekuzi na masuala mengineyo.

Naibu Kamishna wa Polisi wa Somalia Osman Abdullahi Mohamed amewaambia maafisa hao kwamba: "Natumai baada ya kupata mafunzo haya mtawashirikisha na wengine katika mbinu na ujuzi mliopata ili maafisa wengine katika vituo vyenu nao waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi unaotakiwa."

Juhudi za kujenga uwezo wa kuviwezesha vikosi vya usalama vya Somalia kuchukua jukumu kamili la usalama wa nchini mwao wakati ATMIS itakapoondoka Somalia mwezi Disemba 2024 zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live