Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yataka kusitishwa mapigano mara moja Sudan

Sudan Jeshiiii Malalamikp AU yataka kusitishwa mapigano mara moja Sudan

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika (AU) umelaani vikali kuendelea mapigano baina ya majenerali wa kijeshi nchini Sudan na umetoa mwito wa kusitishwa mara moja mapigano hayo na bila masharti yoyote.

Mwito huo umetolewa na Baraza la Amani na Usalama la AU katika taarifa yake ya Jumamosi na baada mkutano wake wa hivi karibunii ambao uliangazia hali ya hivi sasa ya nchi ya Sudan iliyoathiriwa viibaya na mapigano ya ndani.

Sehemu moja ya taarifa hiyo iimesema: Baraza hili linalaani vikali mapiigano yasiyo na msingi yanayoendelea kusababisha uharibifu mkubwa, kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF na Jeshi la Sudan, SAF.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, vita baina ya majenerali wa kijeshi nchini Sudan vimesababisha madhara makubwa kwa usalama na hali ya kibinadamu nchini humo na katika nchi jirani. Maiti zilizoenea kila sehemu kutokana na vita baina ya majenerali wa kijeshi nchini Sudan

Taarifa hiyo ya AU aidha imelaani vikali mauaji ya kiholela ya raia wasio na hatia, uharibifu mkubwa wa miundombinu, ikiwa ni pamoja na majengo ya kidiplomasia, na uporaji wa mali za taifa na raia pamoja na nyanyasaji wa kijinsia wa wanawake na wasichana, na kusema kuwa vitendo vyote hivyo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na za haki za binadamu.

Umoja wa Afrika ambacho ndicho chombo kikubwa zaidi barani Afrika umesisitiza kwenye taarifa yake hiyo kwamba mgogoro wa Sudan hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi na umehimiza kufanyiike mazungumzo ya kweli, ya kina, yenye uwakilishi wa kweli na unaojumuisha pande zote kwani ni kwa njia hiyo tu ndipo Sudan itaweza kuwa na amani na usalama endelevu.

Baraza hilo limesisitizia mwito wake kwa kwa pande zinazozozana "kusitisha mapigano mara moja na bila masharti yoyote na kumaliza mgogoro huo usio na ulazima wowote lazima ambao unaendelea kusababisha hasara kubwa kwa isiyofidika kwa Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live