Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yataka kusitishwa kwa mapigano mara moja yanayoendelea DR Congo

AU Yataka Kusitishwa Kwa Mapigano Mara Moja Yanayoendelea DR Congo AU yataka kusitishwa kwa mapigano mara moja yanayoendelea DR Congo

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: BBC

Umoja wa Afrika umetoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo waasi wamekuwa wakisonga mbele kuelekea mji mkuu wa jimbo hilo mashariki mwa nchi hiyo.

DR Congo imemfukuza balozi wa Rwanda, ikiishutumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao sasa wanautishia mji wa Goma.

Inafuatia utekaji nyara wa waasi wa mji muhimu wa uchukuzi mashariki mwa nchi. Hata hivyo, Rwanda imekanusha mara kwa mara madai kwamba inaunga mkono waasi.

Mji wa Kiwandja uliangukia mikononi mwa waasi siku ya Jumamosi, hiyo ikionesha uwezekano wa kuukata mji mkuu wa kikanda, Goma, kutoka kaskazini mwa jimbo lenye utajiri wa madini la Kivu Kaskazini.

AU imezitaka pande zote kushiriki katika mazungumzo yenye kujenga na inaziita kwenye mazungumzo ya amani nchini Kenya mwezi ujao.

Chanzo: BBC