Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yataka kurejeshwa utawala wa katiba nchi za Gabon, Niger

Wanajeshi Niger AU yataka kurejeshwa utawala wa katiba nchi za Gabon, Niger

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika (AU) ulikariri mwito wake wa kurejeshwa haraka utawala katiba nchini Gabon na Niger kufuatia mapinduzi ya hivi karibuni ya kijeshi katika nchi hizo mbili za barani Afrika.

Mwito huo ambao ndio wa karibuni kabisa kutolewa na Baraza la Amani na Usalama la AU umekuja baada ya mkutano wake wa Jumanne ulioangazia hali ya mambo katika nchi hizo mbili.

Katika taarifa yake kupitia mitandao ya kijamii, Idara ya Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama ya AU imesema: "Baraza limetilia mkazo kuwa haliwezi kuzivumilia kabisa serikali zilizoingia madarakani kinyume na katiba na kusisitizia mwito wake wa kurejeshwa haraka utawala wa katiba katika nchi zote hizo mbili.

Kuhusu hali ya Niger, baraza hilo limetilia mkazo mwito wake wa kuachiliwa mara moja na bila ya masharti rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Bazoum na wafungwa wengine wote na kuheshimiwa haki zao za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na kulindwa afya zao za kimwili na uadilifu wa kimaadili. Wananchi Gabon wakisherehekea mapinduzi ya kijeshi na kupinduliwa utawala wa muda mrefu wa ukoo wa Bongo

Tarehe 26 Julai mwaka huu, jeshi nchini Niger lilifanya mapinduzi yaliyomng'oa madarakani Bazoum na kumchagua Abdourahamane Tchiani, kiongozi wa zamani wa walinzi wa rais wa nchi hiyo, kuongoza Baraza la Taifa la Ulinzi wa Ninger, ambayo ni bodi inayoongoza nchi hiyo hivi sasa. Wananchi wa Niger walikuwa wanamlalamikia sana Bazoum kwa kuwa kibaraka wa kupindukia wa nchi za Magharibi hasa mkoloni kizee wa Ulaya, yaani Ufaransa.

Tarehe 30 Agosti mwaka huu, Brice Oligui Nguema, kamanda mkuu wa Walinzi wa Republican wa Gabon, alitajwa kuwa kiongozi wa mpito wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Baada ya mapinduzi ya kijeshi, AU ilisimamisha uanachama wa nchi za Niger na Gabon hadi pale zitakaporejesha utawala wa katiba.

AU pia iliwataka wahusika wote wa kisiasa, kiraia na kijeshi katika nchi hizo mbili kutoa kipaumbele kwa njia za kuimarisha amani na utatuzi wa kisiasa wa masuala ya nchi hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live