Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yasikitishwa na vitendo vya kigaidi Afrika

Rwanda Imeipiga Ndege Ya Kivita Ya DRC, Kinshasa Imesema Haitaendelea Kuvumilia AU yasikitishwa na vitendo vya kigaidi Afrika

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Umoja wa Afrika (AU) imeelezea kusikitishwa sana na kuendelea kufadhiliwa vitendo vya ugaidi barani Afrika.

Kauli hiyo imetolewa na Baraza la Amani na Usalama la AU katika taarifa yake ya jana kufuatia mkutano wake wa hivi karibuni uliojadili njia za kukabiliana na ugaidi barani Afrika.

Sehemu moja ya taarifa ya baraza hilo la amani na usalama la Umoja wa Afrika imesema: "Baraza linaangalia kwa wasiwasi mkubwa kukendelea kufadhiliwa vitendo vya ugaidi, hususan kuongezeka kwa uhusiano kati ya ugaidi na uhalifu wa kupangwa kimataifa, ikiwa ni pamoja na biashara ya madawa ya kulevya, magendo ya madini na maliasili, pamoja na mtiririko wa fedha haramu na athari zake mbaya kwa uchumi wa nchi wanachama."

Aidha imeeleza kusikitishwa kwake na ongezeko la ukosefu wa amani, usalama na utulivu barani Afrika unaotokana na kuenea vitendo vya kigaidi na itikadi kali za kikatili katika bara zima, jambo ambalo linadhoofisha malengo ya AU ya kunyamazisha milio ya bunduki barani Afrika ifikapo mwaka 2030.

Taarifa hiyo imesisitizia pia azma ya AU ya kufuta kikamilivu ugaidi na itikadi kali za kivita Afrika. Aidha imetoa mwito kwa nchi zote wanachama kujiepusha na maamuzi yoyote yanayopelekea kuchochea, kuhamasisha, kuandaa, kuwezesha, kushiriki katika kufadhili au kuhimiza vitendo vya kigaidi.

Baraza hilo limezihimiza nchi wanachama wa AU kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa maeneo yao hayatumiki katika vitendo vya kigaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live