Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yamteua Adama Dieng mjumbe maalum kupambana na mauaji ya kimbari Afrika

AU Yamteua Adama Dieng Mjumbe Maalum Kupambana Na Mauaji Ya Kimbari Afrika AU yamteua Adama Dieng mjumbe maalum kupambana na mauaji ya kimbari Afrika

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat Jumamosi alimchangua Adama Dieng wa Senegal kama mjumbe maalum wa kwanza wa AU katika kuzuia uhalifu wa mauaji ya kimbari na ukatili mwingine mkubwa.

Kama mjumbe wa AU aliyepewa jukumu hilo, Dieng ataendeleza ajenda za AU kukabiliana na itikadi za chuki na mauaji ya kimbari katika bara la Afrika, Faki alisema katika mtandao wa X ambao awali ulijulikana kama Twitter.

Dieng, aliwahi kufanya kazi kama mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa zamani Ban Ki-moon katika suala la uzuiaji wa mauaji ya kimbari.

Kuteuliwa kwa Dieng kunawadia wakati ambapo AU imepanga kuwa na hafla kubwa yenye uhusiano na maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchi Rwanda.

Kulingana na AU, mwaka 2024 unaashiria ‘’kipindi muhimu kutoa heshima kwa waliopoteza maisha yao, kusimama pamoja na manusura na kuungana pamoja kuzuia ukatili kama huo kutokea tena.’’

Iliongeza kuwa maandamisho hayo ni jukwaa muhimu kuendeleza uelewa kwa watu wa Afrika na jamii ya kimataifa juu ya thamani ya maisha na ubinadamu na kujitolea upya kulinda na kuendeleza haki za kimsingi za binadamu.

Chanzo: Bbc