Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yalaani vitendo vya kuwateka nyara watu nchini Nigeria

Wakimbizi Wa Ndani Watekwa Nyara Nchini Nigeria AU yalaani vitendo vya kuwateka nyara watu nchini Nigeria

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amelaani mashambulizi yanayozidi kuripotiwa kaskazini mwa Nigeria ambapo watoto wadogo na kina mama wamelengwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haramu kwa kutekwa nyara.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Moussa Faki Mahamati amewataka ,‘''waliotekeleza uhalifu huo kuwarejesha watoto waliotekwa mara moja kwa familia zao''.

Ameendelea kusema kwamba, kitendo hicho ni ishara kwamba tishio la ugaidi na wizi wa mifugo ni masuala yanayotishia sio tu usalama wa eneo la kaskazini mwa Nigeria, bali eneo zima na hata mataifa jirani na ni jambo ambalo linasikitisha wote barani Afrika.’

Haya yanajiri wakati ambapo wanafunzi 15 walitekwa nyara Jumamosi, katika eneo la Gada, katika jimbo la Sokoto, kaskazini mwa Nigeria.

Mbunge wa eneo amesema kuwa,shambulizi hilo lilitokea alfajiri, ambapo wapiganaji pia waliwateka wanawake wanne.

Siku ya Alkhamisi wiki iiyopita, wanafunzi takriban 300 walitekwa nyara na wapiganaji waliojihami kwa silaha ambao walitumia pikipiki kushambulia shule ya umma katika jimbo la Kaduna.

Aidha, awali makumi ya wanawake waliokuwa kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la Borno, walitekwa huku mamlaka nchini humo ikihofia kwamba, huenda wakawa watumwa wa wapiganaji wa kundi hilo wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Jeshi la Nigeria linaongoza vikosi vya usalama katika operesheni ya kusawaka mateka hao wanaosemekana kufichwa katika misitu iliyopo kaskazini mwa taifa hilo, huku vifaa kama ndege zisizo na rubani zikitumwa kufanya uchunguzi zaidi katika maeneo yanayojulikana kuwa maficho ya kundi hilo ili kujaribu kuwarejesha watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live