Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yalaani utekaji nyara wanafunzi Nigeria

Wakimbizi Wa Ndani Watekwa Nyara Nchini Nigeria AU yalaani utekaji nyara wanafunzi Nigeria

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani wimbi kubwa la utekaji nyara wa watoto wa skuli na wanawake kwenye maeneo ya kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Taarifa iliyosambazwa jana imesema: "Mwenyekiti wa Tume ya AU analaani vikali wimbi kubwa la utekaji nyara wa watoto wa skuli na wanawake huko kaskazini magharibi mwa Nigeria na anatoa mwito wa kurejeshwa makwao haraka watoto na wanawake waliotekwa nyara.

Ripoti zinasema kuwa, watu wenye silaha waliteka nyara wanafunzi 287 wa skuli katika mji wa Kuriga wa kaskazini magharibi mwa Nigeria siku ya Alhamisi. Huo unahesabiwa kuwa ni utekaji nyara mkubwa zaidi kufanyika kwenye skuli katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Faki Mahamat amelaani utekaji nyara huo uliotokea baada ya genge la watu wenye silaha kuuvamia mji wa Kuriga na kusema kuwa, tukio hilo ni la kigaidi na linaonesha jinsi maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Nigeria yasivyo salama kwa wanawake na wanafunzi wa skuli. Aidha ametahadharisha kwamba kuna hatari athari za vitendo hivyo vya kigaidi zikaonekana kwenye bara zima la Afrika.

Hayo yamekuja baada ya Serikali ya Shirikisho ya Nigeria kuorodhesha skuli kadhaa katika majimbo 14 ya nchi hiyo na kusema kuwa ni maeneo yaliyoko hatarini kushambuliwa na majambazi na wahalifu wenye silaha.

Pamoja na hayo, Hajia Halima Ilya, Mratibu mkuu wa serikali ya Nigeria wa masuala ya skuli zenye usalama; na wala serikali ya Nigeria, hawajataja majina ya majimbo hayo 14 yaliyoripotiwa kuwa yako hatarini kushambuliwa na majambazi na wahalifu wanaobeba silaha.

Idadi ya wanafunzi waliotekwa nyara nchini Nigeria imepindukia 1,400 tangu genge la kigaidi la Boko Haram lilipowateka nyara wanafunzi 276 karibu miaka kumi iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live