Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yalaani ongezeko la mapinduzi ya kijeshi barani Afrika

Mapinduzi Ya Kijeshiiii Yalaaniwa AU yalaani ongezeko la mapinduzi ya kijeshi barani Afrika

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika (AU) umelaani vikali wimbi la mapinjduzi ya kijeshi na kutoheshimiwa katiba linalopelekea kupinduliwa serikali mbalimbali barani Afrika na kukiuka sheria za AU.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU), limesisitizia haja ya dharura ya kuangaliwa upya ufanisi wa AU katika kutatua "janga" hilo.

Baraza hilo limeelezea wasiwasi wake mkubwa kutokana na kuchelewa kurejeshwa utawala wa Katiba katika baadhi ya nchi wanachama wa AU na limesisitizia sana wajibu wa kuongezwa juhudi za kuhakikisha kuwa kazi zote za tawala za mpito katika nchi kunakotokea mapinduzi ya kijeshi, zinatekelezwa kwa muda uliowekwa.

Kauli hiyo ya jana Alkhamisi imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat kulaani mapinduzi ya kijeshi katika nchi ya Afrika ya Kati ya Gabon, ambayo ndiyo nchi ya karibuni kabisa iliyoendelea mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi barani Afrika. Moussa Faki Mahamat

Faki Mahamat amelaani mapinduzi hayo na kuyataja kuwa ni ukiukaji wa wazi wa taratibu zilizowekwa na vyombo vya kisheria na kisiasa vya AU.

Taarifa ya Umoja wa Afrika imeelezea wasiwasi mkubwa wa AU wa kuendelea, kuzuka upya na kuibuka vitisho vya amani na usalama katika bara hilo, vinavyosababishwa na binadamu na matukio ya kimaumbile.

Miongoni mwa vitisho hivyo ni ugaidi, misimamo mikali, mabadiliko ya utawala yaliyo kinyume na katiba, mizozo ya ndani, makundi yenye silaha, kuenea wapiganaji wa kigeni wakiwemo mamluki na magaidi wa kigeni, uhalifu wa kupangwa kimataifa, mtiririko wa fedha haramu na magendo ya maliasili za Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live