Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yakuna kichwa ukiukwaji haki za watoto Afrika

Watoto Mtoto Kijinsia.jpeg AU yakuna kichwa ukiukwaji haki za watoto Afrika

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika (AU) umeelezea kusikitishwa sana na wimbi la kuenea migogoro ya kikatili barani Afrika ambayo inadhoofisha haki za kimsingi na ustawi wa watoto.

Mwito huo umetolewa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika katika taarifa yake ya karibuni kabisa kufuatia mkutano wa hivi karibuni wa baraza hilo ulioangazia njia za kukuza ulinzi wa haki na ustawi wa watoto wanaoishi kwenye migogoro barani Afrika.

Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema: "Baraza hili linatilia mkazo dhamira ya Afrika ya kuendelea kuchukua hatua zinazofaa za kukuza na kulinda haki na ustawi wa mtoto wa Afrika."

Baraza hilo limesisitizia haja ya kupambana vilivyo na ukiukwaji mkubwa wa haki na ustawi wa watoto, ambao ni pamoja na mauaji, kuwasababishia ulemavu watoto, kuandikishwa au kuwatumia watoto katika vita na jeshini, mashambulizi dhidi ya skuli na hospitali, ubakaji na ukatili mwingine mbaya wa kijinsia, utekaji nyara na kunyimwa haki yao ya kufikiwa na misaada ya kibinadamu.

Baraza hilo aidha limetoa mwito kwa nchi wanachama wa AU kuongeza juhudi na kuzingatia zaidi miradi ya ndani ya nchi hizo ambayo itakuza haki na ulinzi wa watoto na kuupa kipaumbele kikubwa utamaduni wa kudhaminiwa usalama wa watoto katika wakati wa amani na wakati wa migogoro.

Mwito wa hivi sasa umetolewa katika hali ambayo, katikati ya mwaka jana na kwenye moja ya ripoti zake za kila mwaka, Umoja wa Afrika ulitangaza kuwa, robo ya wakazi wa eneo la Sahel Afrika hasa watoto wadogo, hawapati huduma muhimu za afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live