Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yaja na mwarobaini unyanyasaji wa kijinsia

Unyanyasaji Kijinsia AU yaja na mwarobaini unyanyasaji wa kijinsia

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika (AU) umesisitizia haja ya kuongezwa juhudi za makusudi za kuhakikisha wanawake wanawezeshwa kiuchumi ili kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

Katika taarifa yake, AU imesema unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana ni ukiukaji wa kimsingi wa haki za binadamu na unaathiri vibaya ustawi wa mtu binafsi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, ni jambo la msingi kuweko mabadiliko ya kijamii na kisheria kwa ajili ya kuweka mazingira wezeshi ya kuboresha usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa wanawake kifedha kama hatua ya kuzuia na kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

AU imetoa mfano wa utafiti wa hivi karibuni wa Shirika la Kazi Duniani na Umoja wa Wanawake wa Umoja wa Mataifa na kusema kuwa, ukatili dhidi ya wanawake na wasichana hubeba gharama kubwa ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na upungufu wa wafanyakazi, kupungua uzalishaji kwa kutotumiwa vizuri nguvukazi ya wanawake na hasara yanayopata makampuni kutokana na viwango vya juu vya utoro makazini.

AU yataka kuwezeshwa kiuchumi wanawake ili kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Mwito huo umetolewa kabla ya mkutano ujao wa AU wenye mada ya kuwawezesha wanawake ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 30 na 31 huko Moroni, mji mkuu wa Comoro.

Mkutano huo ulioitishwa chini ya kaulimbiu "Kutekeleza Ahadi Kuelekea Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi na Kukomesha Unyanyasaji Dhidi ya Wanawake na Wasichana," pamoja na mengine, utatafuta masuluhisho ya kiubunifu na ya kivitendo na kuwarahisishia wanawake ufadhili na mikopo, uhamishaji fedha, chakula cha msaada na kuvisaidia vikundi vya wanawake na mitandao ya wajasiriamali wanawake.

Agenda 2063 ya AU imekusudiwa kuunda Afrika ambayo maendeleo yake yataendeshwa na watu wenyewe, yakitegemea uwezo wa watu wa Afrika, hasa wanawake na vijana, pamoja na kutunza watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live