Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yaizuia Israel kuingia Makao yake Makuu

Umoja Wa Afrika AU AU AU yaizuia Israel kuingia Makao yake Makuu

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chanzo cha kidiplomasia cha Afrika kimeiambia televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwamba Umoja wa Afrika umewazuia wajumbe wa utawala ghasibu wa Israel kuingia katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, ambao walikuwa wameomba kukutana na maafisa wa Afrika kwa madhumuni ya kuwasilisha maoni ya serikali ya Tel Aviv kuhusu vita vinavyoendelea huko Gaza.

Wanadiplomasia wanasema, ujumbe wa Israel uliojumuisha Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Yaakov Blichstein, na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Afrika, Amit Bias, ulifika Addis Ababa na kujaribu kushiriki katika ufunguzi wa kikao cha mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika kama waangalizi, lakini Umoja wa Afrika umewazui kuingia kwenye mkutano huo.

Ripoti zinasema kuwa ujumbe huo ulikuwa unataka kuwasiliana na maafisa kadhaa wa Afrika, ili kupunguza ukali wa msimamo wa nchi za bara hilo dhidi ya Israel kutokana na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo katika vita vya Gaza, na vilevile kujaribu kuzishawishi baadhi ya nchi kuunga mkono uanachama wa Israel katika Umoja wa Afrika kama mwangalizi baada ya kukataliwa matakwa ya awali ya utawala huo.

Inafaa kuashiria kuwa, ujumbe wa Israel ulijaribu kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Afrika uliofanyika Addis Ababa mwezi Februari mwaka jana, lakini umoja huo ulikataa kutokana na pingamizi la nchi kadhaa za Afrika, zikiongozwa na Afrika Kusini na Algeria.

Mjadala wa kutambuliwa Israel kama mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika ulianza Julai mwaka jana wakati Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, alipoupatia utawala huo haramu hadhi ya kuwa mwanachama mwangalizi katika umoja huo na kusababisha mzozo mkubwa ndani ya chombo hicho.

Nchi nyingi za Kiafrika zinaitambua hatua ya Moussa Faki Mahamat ya kuukubali utawala wa Kizayuni katika Umoja wa Afrika kama mwanachama mwangalizi kuwa ni kuyasaliti mapambano ya kupigania uhuru ya Palestina.

Umoja wa Afrika (AU) ulisimamisha nafasi ya mwanachama mwangalizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika umoja huo kutokana na upinzani mkali wa nchi nyingi zikiongozwa na Algeria na Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live