Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yaiunga mkono UN kuhusu Palestina

Wapalestina 4,651 Wameuawa Katika Vita AU yaiunga mkono UN kuhusu Palestina

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika ametangaza uungaji mkono wake kamili kwa Kaitbu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kutokana na 'uongozi na msimamo wake imara' kuhusu hujuma ya kijeshi ya utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza.

Moussa Faki Mahamat ameandika katika ukurasa wake wa X kwamba: "Naunga mkono kikamilifu uongozi na msimamo imara wa Antonio Guterres na kazi ya Umoja wa Mataifa katika Ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa Mabavu."

Katika hotuba yake mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Matafa siku ya Jumanne, Guterres alilaani mashambulizi yaliyotekelezwa na Hamas Oktoba saba lakini akasisitiza kwamba hayakufanyika bila sababu.

Guterres amesema: "Hali katika Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) inazidi kuwa mbaya na huenda vita vya Ghaza vikaenea katika eneo hilo. Kuua raia sio jambo la kuhalalishika hata kidogo. Shambulio la Hamas halikufanyika bila sababu na wananchi wa Palestina wanakabiliwa na mzingiro mkali. Mchakato wa ujenzi wa viitongoji vya walowezi wa Kizayuni unamega na kumeza ardhi za Palestina na kuteketeza malengo ya Wapalestina. Mashambulizi yasiyokoma na mashambulizi makali ya Israel dhidi ya Ghaza yanaendelea kwa njia ya kutisha."

Israel imeonyeshwa kuchukizwa mno na misimamo hiyo ya Antonio Guterres katika hali ambayo, kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa hajaonyesha isipokuwa sehemu ndogo sana ya hali ya kusikitisha na ya maafa ya vita vya Ghaza na mazingira yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live