Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yaamua kutumia upatanishi utatuzi migogoro ya ndani

Marekani Inaitaka RSF Ya Sudan Kuacha Kushambulia Maeneo Ya Raia AU yaamua kutumia upatanishi utatuzi migogoro ya ndani

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikao cha siku mbili cha nchi za Afrika kilichoanza siku ya Jumatano jijini Nairobi Kenya, kimefikia uamuzi wa kuendeleza kutumia upatanishi chini ya mwavuli wa mahakama kutatua migogoro ya kisheria barani Afrika.

Mkutano huo wa Usuluhishi baina ya Mabara umewaleta pamoja zaidi ya maafisa 100 wa mahakama na wapatanishi kutoka kote barani Afrika ili kubadilishana mawazo na kujadiliana kuhusu jinsi ya kukuza njia ya upatanishi kama chaguo la kwanza katika utatuzi wa migogoro.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Bi Martha Koome, Jaji Mkuu na ambaye pia ni Mkuu wa Mahakama ya Kilele ya Kenya, amesema kuwa, upatanishi unaoendeshwa chini ya vigezo na vielelezo vya mahakama ni sehemu ya njia ya haki yeye milango mingi kwa sababu ndani yake mna ubunifu mwingi ambao unaweza kuisaidia bara la Afrika kuongeza ufanisi kwenye mifumo yake ya kutoa maamuzi ya haki.

Vile vile amesema, suala la mahakama kuingilia masuala kama ya malezi ya mtoto, matunzo na kutatua migogoro mingine ya kifamilia linapaswa kuwa suluhisho la mwisho, na kwamba kuna wajibu wa kuufanya upatanishi kutangalia maamuzi ya mahakama katika mizozo hiyo. Nchi za Afrika zafadhalisha kutatua matatizo kwa upatanishi kabla ya kufikia ngazi ya Mahakama

Naye Harriet Magala, Jaji wa Mahakama Kuu nchini Uganda, amesema kwenye mkutano huo wa siku mbili wa jijini Nairobi Kenya kwamba, mahakama za Afrika zinapaswa kupiga hatua katika kutumia upatanishi kama njia mbadala ya kutatua migogoro na kukuza utamaduni wa upatanishi katika utatuzi wa migogoro na mizozo mingi barani humo.

Naye Elachi Agada, Mkuu wa Taasisi ya Wapatanishi ya Nigeria amesema kwenye mkutano huo kwamba bara la Afŕika linaweza kutumia upatanishi kuhakikisha kuwa mifumo ya sheŕia yenye ufanisi na usawa kwa wote inapatikana, inaheshimiwa na kutekelezwa kivitendo.

Aidhaa ametaka Afrika izingatie utatuzi wa migogoro ya kibiashara, ardhi na ajira kwa njia ya upatanishi, kwani migogoro hiyo inaweza kuwa na madhara makubwa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na shirikishi ya bara hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live