Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yaahirisha mjadala kuhusu hadhi ya Israel

AU ISRAEL AU yaahirisha mjadala kuhusu hadhi ya Israel

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika umeahirisha mjadala kuhusu kuiondolea Israel hadhi ya kuwa mtazamaji kwenye Umoja huo. Hatua hiyo imeepusha upigaji kura ambao ungeleta mpasuko katika Umoja huo wa nchi wanachama 55.

Haya ni kwa mujibu wa wanadiplomasia walioliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, katika siku ya mwisho ya kikao cha kila mwaka cha Umoja huo mjini Addis Ababa,

Mmoja wa wanadiplomasia aliliambia shirika hilo la AFP kwamba suala hilo la Israel limeahirishwa kwa sasa na badala yake, kutaundwa kamati kulichunguza.

Kamati hiyo ya nchi sita ni pamoja na Afrika Kusini, Algeria, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Cameroon na Nigeria.

Wanadiplomasia hao wamesema ratiba ya kazi ya kamati hiyo haijatolewa na pia haijaelezwa ni lini Umoja wa Afrika utalishughulikia suala hilo tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live