Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU kusaidia upatikanaji wa amani ya kudumu nchini Somalia

AU SOMALIAAAAA AU kusaidia upatikanaji wa amani ya kudumu nchini Somalia

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa Taasisi ya AUCF ya Umoja wa Afrika ambao kazi yake ni kusaidia kupatikana amani ya kudumu na kuimarisha sheria za kimataifa, umeitembelea Somalia ili kuimarisha juhudi za ulinzi wa raia kabla ya kipindi cha mpito.

Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kilitangaza jana Jumatano kwamba ujumbe huo unaoongozwa na mratibu wa AUCF Adebayo Kareem umefanya mazungumzo na Kamanda wa Kikosi cha AMIS Sam Okiding, uongozi wa kitengo cha kijeshi na makamanda wa sekta mbalimbali na maudhui kuu ilikuwa ni jinsi AU inavyoweza kusaidia kuchungwa sheria na kupatikana amani ya kudumu huko Somalia.

Taarifa ya ATMIS mjini Mogadishu, mji mkuu wa Somalia imesema: "Majadiliano hayo yalilenga kutekeleza na kuzingatia Kanuni za Ushirikiano za Umoja wa Afrika zilizofanyiwa marekebisho hivi karibuni ambazo sasa zinawiana na mamlaka iliyopewa ATMIS ili kuimarisha juhudi za ulinzi wa raia."

Tarifa hiyo imeongeza kuwa, kama sehemu ya ziara yao ya wiki moja nchini Somalia, ujumbe huo utashirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo maafisa wa serikali, ATMIS, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia ili kuimarisha zaidi ulinzi wa raia wakati huu wa mchakato wa mpito nchini Somalia.

Miongoni mwa malengo ya timu ya AUCF ni kuimarisha uwezo wa Umoja wa Afrika wa kuhakikisha kuwa shughuli za usaidizi wa amani za chombo hicho kikubwa zaidi barani Afrika zinapangwa na kuendeshwa kwa kufuata sheria za kimataifa za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na sheria za kikanda za haki za binadamu pamoja na viwango vinavyotumika kimataifa vya kimaadili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live