Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU: Vita vya Israel dhidi ya Gaza haviwezi kutetewa

Israel Yasema Wanajeshi Wake Wako 'katika Kitovu Cha Mji Wa Gaza' AU: Vita vya Israel dhidi ya Gaza haviwezi kutetewa

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amesema vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza ni vita ambavyo haviwezi kutetewa hata kidogo kwa kisingizio chochote kile.

Kwa mujibu wa IRNA, Assoumani Azali mkuu wa muda wa Umoja wa Afrika, alisisitiza Jumatatu katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, mji mkuu wa Ujerumani, kwamba jibu la Israel kwa operesheni za Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas) halina uhalali.

Azali, ambaye pia ni rais wa Visiwa vya Komoro amelaani jibu la utawala wa Kizayuni kwa oparesheni ya Hamas ya tarehe 7 Oktoba.

Ameongeza kuwa: "Tunalaani hatua zote, vitendo vyote, kila kitu kinachodhuru watoto na ambacho kinasababisha watu wenye msimamo mkali wanapopatwa na jambo kama hilo."

Rais Azali alikuwa akijibu swali wakati wa mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat.

Cyril Ramaphosa, rais wa Afrika Kusini siku ya Jumatano pia alitaja vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza kuwa ni jinai ya kivita na akatangaza kuwa nchi yake na nchi zingine kadhaa zitafikisha mashhtaka dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Muendelezo wa vita vya maangamizi ya umati dhidi ya Ukanda wa Ghaza na mauaji ya wanawake na watoto wa Kipalestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni yanajiri huku nchi za Magharibi zinazouunga mkono utawala huo hasa Marekani na Uingereza zikipiga kura ya turufu dhidi ya azimio lolote la usitishaji vita katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na badala yake zinataka kupitishwa maazimio yanayounga mkono zaidi Tel Aviv.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live