Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATMIS kuimarisha usalama Somalia

Marekani Yauwekea Vikwazo Mtandao Wa Kiislamu Wa Somalia ATMIS kuimarisha usalama Somalia

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kimetangaza kuwa kimeweka mikakati imara ya kuimarisha usalama katika kona zote za Somalia wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Afrika nchini Somalia Mohamed, El-Amine Souef ametoa mwito kwa wananchi wote wa Somalia kushirikiana na vikosi vya kulinda usalama vya nchi hiyo na kile cha ATMIS ili kuhakikisha usalama wa umma unalindwa zaidi ndani ya mwezi huu mtukufu.

Ameongeza kuwa, ushirikiano kati ya vikosi vya kulinda usalama na wananchi wa Somalia ni muhimu katika kuepusha mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa mara kwa mara na magaidi wa al Shabab ambao hawaheshimu matukufu ya kibinadamu na Kiislamu ukiwemo mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mwezi Mtukufu wa Ramadhani una nafasi kubwa na muhimu sana kwa Waislamu wakiwemo wa Somalia

Vilevile amesema: "Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ATMIS inaahidi kuendelea kutimiza wajibu wake wa kuvisaidia vikosi vya kulinda usalama vya Somalia ili kuhakikisha amani na usalama wa watu wa Somalia unadumishwa pamoja na mali zao katika maeneo ambayo usalama wake unasimiwa na timu hiyo ya Umoja wa Afrika huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

Uzoefu unaonesha kuwa magaidi wa al Shabab huwa wanazidisha mashambulizi yao ya kigaidi wakati wa Ramadhani na wanashambulia zaidi maeneo ya mijini, kambi za kijeshi na maeneo mengine ya umma kama vile mahoteli, masoko na mikahawa yenye shughuli nyingi.

Vitendo hivyo vya kigaidi vya al Shabab ambavyo vinalenga kuwakosesha utulivu Waislamu ndani ya mwezi muhimu na mtukufu sana wa Ramadhani, vimekuwa vikilaaniwa mno duniani hasa kwa kuzingatia kuwa mwezi wa Ramadhani una nafasi ya kipekee nchini Somalia na Waislamu wanatumia siku na mikesha ya mwezi huo kwa ibada, kuhudhuria kwa wingi Misikitini n.k.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live