Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AS Kigali ruksa kufanya mazoezi

9063f0e92a341abb5af33664bda569de AS Kigali ruksa kufanya mazoezi

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAWAKILISHI wa Rwanda katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, AS Kigali imehakikishiwa ruhusa maalum kuendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya kukabiliana na CS Sfaxien, imeelezwa.

“Naweza kuthibitisha kuwa tumepewa ruhusa na Wizaya ya Michezo kuendelea na mazoezi yetu dhidi ya CS Sfaxien. Jumatatu (jana) ndio tutaanza mazoezi yetu, “alisema Francis Gasana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo juzi.

Kigali kwa sasa wako katika utaratibu wa kutotoka nje wakati serikali ikiangalia utaratibu wa kupambana na Covid-19.

Mashindano makubwa ya soka kwa sasa yamesimamishwa, ikiwa ni miongoni mwa matukio mengine ya michezo.

Baada ya kupewa ruhusa ya kuendelea na mazoezi, AS Kigali inatarajia kuweka utaratibu kabambe wa mazoefu unaofuata kanuni zilizowekwa na serikali kwa ajili ya kujikinga na Covid-19.

Timu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Kigali imewafanya mashabiki wake kutembea kifua mbele hadi sasa wakati wakikaribia kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika.

Hadi sasa timu hiyo imeitoa klabu ya Botswana ya Orapa United, na ile ya Uganda ya KCCA FC.

Kwa sasa wanakabiliana na kazi ya kukiweka fiki kikosi chao ili kukabiliana na klabu ya Tunisia ya CS Sfaxien wakati wakiwa na matumaini ya kupenya hadi hatua ya makundi.

AS Kigali watasafiri kuifuata Sfaxien kwa ajili ya mchezo wa kwanza Jumapili Februari 14.

Timu hizo mbili zitapambana tena wiki moja baadae katika mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Stade de Kigali Jumapili ya Februari 21.

Katika mechi hizo mbili, timu hiyo ya Kigali itacheza bila wachezaji wake watano ambao wako katika majukumu ya timu ya taifa katika mashindano yanayoendelea ya Mataifa ya Afrika (Chan) huko Cameroon.

Wachezaji hao ni Muhadjiri Hakizimana, Eric Nsabimana, Kalisa Rachid, Eric Ndayishimiye na Emery Bayisenge.

Chanzo: habarileo.co.tz