Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ANC chawasiliana na wapinzani kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

ANC Chawasiliana Na Wapinzani Kuunda Serikali Ya Umoja Wa Kitaifa ANC chawasiliana na wapinzani kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Voa

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) Jumatano kilisema kimewasiliana na wapinzani ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, baada ya kushindwa kupata wingi wa kura katika uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita.

Hesabu ya mwisho ya kura ilionyesha chama cha Rais Cyril Ramaphosa kilipata wabunge 159 katika Bunge la taifa lenye viti 400, chini ya wabunge 230 na ulikuwa ushindi mdogo sana wa ANC katika uchaguzi mkuu.

Msemaji wa ANC Mahlengi Bhengu-Motsiri aliwambia waandishi wa habari kwamba chama chake kilifanya mazungumzo “ya kiuchunguzi” na vyama vingine kadhaa, huku kikijarabu kupata uungwaji mkono wa kutosha wa wabunge kuunda serikali na kumchagua rais.

Baraza la ANC la kufanya maamuzi linatarajiwa kukutana leo Alhamisi ili kuhakiki njia zote, ikiwemo kujaribu kuunda serikali ya wachache, alisema.

Lakini majadiliano yalijikita kwenye “serikali ya umoja wa kitaifa” kwa sababu hiki ndicho wananchi wa Afrika Kusini walichotuomba, aliongeza.

Chanzo: Voa