Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AHUKUMIWA KIFO KWA KUKUFURU DINI

Kitanzi AHUKUMIWA KIFO KWA KUKUFURU DINI

Tue, 11 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mwanamuziki nchini Nigeria katika jimbo la kaskazini la Kano amehukumiwa kifo kwa kunyongwa baada ya kuikufuru imani ya dini ya Kiisilamu.

Mahakama ya juu ya kiislamu inayotumia Sheria ya kiislamu katika eneo la Hausawa Filin Hockey katika jimbo la Kano imesema kuwa Yahaya Sharif-Aminu, mwenye umri wa miaka 22, alipatikana na hatia ya kukufuru kwa wimbo wake uliosambazwa kupitia mtandao wa WhatsApp mwezi Machi, Mtuhumiwa huyo Bwana Yahaya Sharif-Aminu hakukanusha mashitaka alipoulizwa.

Wakosoaji wanasema wimbo huo ulikufuru kwani ulimsifu imam wa Waislam wa Tijaniya kiasi kwamba ulimpatia hadhi ya juu kuliko Mtume Muhammad (saw)

Waandamanaji walikua wamechoma moto nyumba ya familia yake na kukusanyika nje ya makao makuu ya polisi ya kiislamu huku Hisbah, wakidai hatua ichukuliwe dhidi ya mtuhumiwa huyo.

Mwanamuziki huyo ambaye alikua amejificha baada ya kutunga wimbo huo kwa sasa anashikiliwa na polisi ili kusubiri hukumu ipite.

Chanzo:BBC

Chanzo: zanzibar24.co.tz