Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

A.Kusini: Wafanyakazi mgodini waendelea kusota chini ya ardhi

Mgodiniii Afrika Kusini (600 X 310) A.Kusini: Wafanyakazi mgodini waendelea kusota chini ya ardhi

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wafanyakazi 500 katika mgodi mmoja nchini Afrika Kusini, wameendelea kusota chini ya ardhi tangu Jumapili katika kile kinachodaiwa kuwa ni mzozo kati ya vyama viwili vya wafanyakazi.

BBC imeripoti kuwa Chama cha Kitaifa cha Wafanyakazi wa Migodi (Num) kilisema wafanyakazi katika mgodi wa One Gold Modder East karibu na Jiji la Johannesburg walikuwa wanazuiliwa chini ya ardhi kinyume na matakwa yao.

Taarifa ya Num imesema: "NUM inatoa wito kwa vyombo vya kutekeleza sheria nchini Afrika Kusini kuingilia kati na kwenda chini kuwakamata "wahuni" wanaowashikilia wanachama wetu kinyume na matakwa yao."

Kwa upande mwingine, Chama cha Wafanyakazi wa Migodi na Ujenzi (Amcu), kimesema wafanyakazi wengi walikuwa wakifanya maandamano kushinikiza mgodi huo kuitambua Amcu.

Wawakilishi kutoka katika mgodi huo wameomba amri ya mahakama ili kukomesha kile ambacho wamekielezea kama "kusalia chini ya ardhi kinyume cha sheria."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live