Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

90% ya vifo vya Corona Zimbabwe ni ya wasiopata chanjo

Jm Waziri wa Afya , John Magwiro

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia repoti ya Afya zimbwabwe inasema takribani asilimia 90% ya waliofariki na virusi vya corona walikuwa hawajapata Chanjo.

Waziri wa Afya nchini humo Dr John Mangwiro amesema kuna faida kubwa ya Chanjo kwenye serikali, ameyasme hayo Septemba 8, huku akiwahimiza wananchi waendlea kujitokeza kwenye vituo vya Afya kupata chanjo.

"Kulikuwa na miili ya watu 207 waliofariki na corona na watafiti wetu walitumia miili hiyo kufanyia uchunguzi na wakabaini kuwa asilimia 90% walikuwa hawajapata chanjo ya corona hivyo nendeni mkachanje mjiepushe na kifo." , amesema Dr. Mangwiro

Dr Mangwiro ameendelea kusisitia kuwa chanjo inauwezo mkubwa wa kutengeza na kuhimarisha kinga ya mwili .

Hata hivyo, zaidi ya watu million 1.7 wameshapata chanjo nchini zimbwabwe na wanatarajia idadi itazidi kupanda ndani ya siku 30.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live