Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

60,000 kupatiwa chanjo dhidi ya kipindupindu

A6aeafdd9bb5eef48b4b100dae2f5364 60,000 kupatiwa chanjo dhidi ya kipindupindu

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATU zaidi ya 60,000 wanatarajia kupatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu katika kampeni maalumu iliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Busia, Kapteni Chris Okiria hivi karibuni.

Wilaya ya Busia inakabiliwa na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa kipindupindu. Kaimu Ofisa Afya wa Wilaya hiyo, Dk Wills Syongola alisema pamoja na mlipuko huo hali haijawa mbaya kama ile ya mwaka 2017.

Mlipuko wa mwaka huo ulisababisha vifo sita kati ya watu 100 walioambukizwa ugonjwa huo. Alisema kwamba chanjo kama hiyo imekuwa ikitolewa katika wilaya za Kasese, Ntoroko, Hoima na Namayingo.

Mwenyekiti wa wilaya ya Busia, Geoffrey Wandera alipongeza wadau mbalimbali kwa kuhamasisha wananchi wa maeneo hayo kukabiliana na ugonjwa huo kwa kupata chanjo.

Alibainisha kuwa kiwango cha upatikanaji wa maji safi na salama katika wilaya hiyo ni asilimia 75 na kutaka wakazi wake kuacha kujisaidia maeneo ya wazi.

Chanzo: habarileo.co.tz