Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

448 wauawa katika maandamano: IHR

000 32NV2ZB 1024x640 448 wauawa katika maandamano: IHR

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Dar24

Shirika la kutetea haki za binadamu, la Iran (IHR), limesema watu 448 waliuawa na vikosi vya usalama nchini Iran katika harakati za kuyakabili maandamano yaliyoanza katikati ya mwezi Septemba, 2022.

Shirika hilo limesema, nusu ya watu hao (224), wameuwawa katika maeneo ya jamii za makabila ya walio wachache tangu kuanza kwa maandamano hayo.

Kwa mujibu wa shirika hilo lenye makao yake nchini Norway, kati ya watu hao 448 waliouliwa, 60 walikuwa ni watoto chini ya umri wa miaka 18 wakiwemo wasichana tisa na wanawake 29.

Awali, Brigedia jenerali. Amirali Hajizadeh kutoka jeshi la kimapinduzi la jamhuri hiyo ya kiislamu alisema zaidi ya watu 300 waliuawa, ikiwa ni kauli ya kwanza ya mamlaka kukiri kuhusu idadi ya waliouwawa.

Chanzo: Dar24