Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

40 wafariki kwenye mapigano Ethiopia

Ethiopia Mapoigano 2323 40 wafariki kwenye mapigano Ethiopia

Thu, 16 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 40 wameuawa na wengine 35 wamejeruhiwa katika mji wa magharibi mwa Ethiopia wa Gambella katika makabiliano baina ya wajumbe wa makundi yaliyofanya mashambulizi Jumanne, maafisa wa ngazi ya juu katika jimbo hilo wameiambia BBC.

Kulingana na mmoja wa maafisa hao kumi kati ya waliouawa walikuwa na wanajeshi wa usalama wa serikali .

Msemaji wa kikundi cha Oromo Liberation Army (OLA) amesema kwamba kikundi hiki kilianzisha ‘opesheni’katika mji huo kwa ushirikiano na makundi yanayotaka kukombolewa kwa Gambella- Gambella Liberation Front.

Baadaye msemaji alisema ‘operesheni’ ilikamilika ‘baada ya kufikia malengo yake’ na kuongeza kuwa ‘kiasi kikubwa’ cha silaha kilikamatwa.

Wakazi wameiambia BBC kuwa hali ya utulivu inaonekana kurejea tena katika mji huo Jumatano, lakini biashara bado zimefungwa. Jumanne jioni rais wa jimbo hilo alikuwa amesema vikosi vyake vimeudhibiti mji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live