Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

40,000 wahudhuria kuapishwa kwa Mnangagwa Zimbabwe

40,000 Wahudhuria Kuapishwa Kwa Mnangagwa Zimbabwe 40,000 wahudhuria kuapishwa kwa Mnangagwa Zimbabwe

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: Voa

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameapishwa Jumatatu kuhudumu kwa muhula wa pili baada ya uchaguzi uliozua utata, ambapo aliibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa.

Inakadiriwa watu elfu 40, walimshangilia Mnangagwa alipowasilil kweye uwanja wa taifa wa michezo mjini Harare. Katika hotuba yake, aliwashukuru wazimbabwe kwa kile alichokiita kuwa uchaguzi wa amani na uwazi.

Aliahidi kutumia rasilimali za asili za Zimbabwe ili kuongeza uzaishaji na kuugeuza uchumi wa nchi.

Mnangagwa anaonekana kuwa ana kibarua kizito mbele yake, wakati taifa lake likikabiliwa na mfumuko mkubwa sana wa bei duniani, na kuwa na safaru ambayo inakaribia kutokuwa na dhamani kabisa. Katika sherehe hizo Mnangagwa, alipigiwa mizinga 21 na kikosi cha wanajeshi wa Zimbabwe, kuashiria mwanzo wa mhula mpya wa Mnangagwa

Kiongozi huyo aliingia madarakani kwa mara ya kwanza 2017 baada ya kumuondoa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, na kisha baadaye akashinda kwenye uchaguzi uliozua utata mwaka uliofuata.

Katika uchaguzi wa mwezi uliopita, mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 80 alimshida mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa mwenye umri wa miaka 45, kutoka chama cha Citizens Coalition for Change, CCC, kulingana na matokeo ambayo sasa yanapingwa na upinzani.

Kiongozi wa chama cha CCC Tendal Biti amesema kwamba anaona hatari mbele iwapo matokeo ya uchaguzi huo hayatabatilishwa.

Chanzo: Voa