Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

30 wahukumiwa kifo DRC

40abe540db35de6a73afe1773af9f1a9.jpeg 30 wahukumiwa kifo DRC

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATU 30 wamehukumiwa kifo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), baada ya kupatikana na hatia ya kusababisha machafuko siku ya Alhamisi Mei 13 mwaka huu, wakati wa Swala ya Kumaliza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Raamadhani.

Kesi hiyo ilisikilizwa kwa siku moja na kutolewa hukumu kwa watu hao baada ya kupatikana hatia za kuchochea machafuko wakati Waislamu wanamaliza Mwezi wa Ramadhani na kukaribisha Sikukuu ya Eid.

Polisi mjini Kinshasa, Sylvano Kasongo, alisema vurugu hizo zilisababisha kifo cha askari polisi mmoja na wengine 40 kujeruhiwa. Hata hivyo, watu 35 walitiwa mbaroni kwa kusababisha mashafuko hayo.

Ilielezwa kuwa, machafuko hayo yalianza baada ya makundi mawili ya Kiislamu kutofautiana kuhusu ni nani atoe swala ya kumaliza mfungo huo na kukaribisha Sikukuu ya Idd.

Kwa mujibu wa tarifa kutoka Kinshasa, hukumu hiyo ilitolewa juzi mjin humo.

Licha ya hukumu hiyo, tangu mwaka 2003, DRC haijatekeleza hukumu ya kifo kwa watu wanaotiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo, bali hutumikia kifungo cha maisha gerezani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz