Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

22 wafariki boti ikizama Bahari ya Hindi

Madagascar Pic Hnnjk 22 wafariki boti ikizama Bahari ya Hindi

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wahamiaji 22 wamefariki baada ya mashua iliyokuwa imebeba watu 47 kuzama katika pwani ya Madagascar wakati ikielekea Kisiwa cha Mayotte.

Shirika la Usafiri wa Baharini la Madagascar limesema watu 23 wameokolewa huku juhudi za kuwatafuta wengine wawili zikiendelea.

Shirika hilo limesema ajali hiyo imetokea juzi Jumamosi ambapo wahamiaji hao walikuwa wamechukua mashua kwa siri kuelekea hadi Mayotte.

Wengi wa waliookolewa wamekimbia ili wasikamatwe, Shirika la Babari la Reuters lilimnukuu ofisa wa polisi akisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live