Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

2023 Tajiri Jack Ma 'kufundisha katika chuo kikuu cha uongozi cha Rwanda'

2023 Tajiri Jack Ma ' Kufundisha Katika Chuo Kikuu Cha Uongozi Cha Rwanda' 2023 Tajiri Jack Ma ' kufundisha katika chuo kikuu cha uongozi cha Rwanda'

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Chuo kikuu cha masuala ya uongozi cha kiafrika- African Leadership University (ALU) kimetangaza kuwa tajiri Mchina Jack Ma ambaye ni muasisi wa kampuni ya biashara ya mauzo ya mtandaoni- Alibaba Group, amechaguliwa kuwa mwalimumgeni katika chuo hicho kilichopo mjini Kigali.

Tovuti ya Chuo hicho kikuu inamnukuu, muasisi wake, Dr Fred Swaniker, akisema kuwa amefurahiakuwa wawekezaji vijana wa Afrika wanaosomea katika chuo hicho“sasa watapata fursa ya kufunzwa na mmoja wa wawekezaji wakubwa zaidi duniani”.

Jack Ma – ambaye wakati mmoja alikuwa ndiye mtu tajiri zaidi nchini China – anaripotiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na uongozi wa Uchina baada ya kukosoa baadhi ya utendaji wake.

Jack Ma binafsi hajadhibitisha wazi madai ya chuo hiki cha kibinafsi, lakini , hivi karibuni ulitangaza kuwa Ma anarejea tena ‘’kufanya mambo aliyanayoyapenda” – kufundisha – kazi “aliyokuwa akiifanya kabla ya kuanzisha kampuni ya Alibaba”.

Chanzo: Bbc