Watu 20 wabaripotiwa kupoteza maisha yao katika ajali mbaya ya barabarani baada ya basi walimokuwa wakisafiria kugongana dafrau na lori ya kusafirisha hela nchini Afrika Kusini.
Kulingana na taarifa kutoka Johannesburg, watu wengine Zaidi ya 60 walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo mbaya.
"Watu 20 walikufa kwa kusikitisha katika ajali baada ya lori la kusafirisha pesa kupoteza mwelekeo na kuanguka uso kwa uso na basi lililokuwa likienda upande mwingine" idara ilisema katika taarifa kama ilivyonukuliwa.
Kumi kati ya waliojeruhiwa walikuwa katika hali mbaya na walisafirishwa hadi hospitali. Polisi wapiga mbizi walikuwa wakipekua mto unaopita kando ya barabara kuu "kutafuta watu wengine ambao huenda walifagiliwa."
Chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa, lakini mvua kubwa imekuwa ikinyesha eneo hilo katika siku za hivi karibuni, msemaji wa idara hiyo, Tidimalo Chuene, aliiambia AFP.
Mvua kubwa imesababisha mafuriko katika mikoa kadhaa ya nchi hiyo katika siku chache zilizopita. Takriban watu saba wameuawa, jambo ambalo pia lilisababisha serikali inayoongoza kutangaza kuwa ni janga la kitaifa.
Kulingana na taarifa ya idara usalama barabarani eneo la Limpopo, lori hilo lilipoteza mwelekeo na kuligonga basi la abiria ambalo lilipepea na kuanguka kwenye daraja lililokuwa katika barabara hiyo.