Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

18 wapoteza maisha, maelfu wakosa makazi kimbunga Madagascar

Kimbungaaaaa 18 wapoteza maisha, maelfu wakosa makazi kimbunga Madagascar

Sun, 31 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kimbunga cha kitropiki kilichoikumba Madagascar kimesababisha vifo vya watu wasiopungua 18 na wengine kadhaa kutoweka baada ya kupiga eneo la kaskazini mwa kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi mapema wiki hii.

Taarifa za hivi punde zimebaini kuwa kimbunga hicho kimesababisha mafuriko makubwa, na kuwacha takriban watu 47,000 wakilazimika kuhama makao yao. Aidha kimbunga hicho kimsababisha maporomoko ya ardhi yaliyopelekea watu kadhaa kujeruhiwa.

Ofisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Maafa imesema kimbunga hicho kiliambatana na upepo mkali wa wastani wa kasi ya kilomita 150 kwa saa.

Picha za angani zilionyesha makazi yaliyojaa maji, huku watu wakijaribu kuwaokoa wakaazi kutoka kwenye nyumba zilizofurika maji.

Kimbunga Gamane kilipiga kaskazini mwa Madagaska siku ya Jumatano na kuacha nyuma uharibifu mkubwa.

Madagascar imekumbwa na angalau vimbunga 10 vikali vya kitropiki tangu mwanzoni mwa 2022, na inakabiliwa na baa la njaa katika baadhi ya maeneo kutokana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.

Umoja wa Mataifa unasema Madagascar imekabiliwa na idadi kubwa ya vimbunga katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, sambamba na kustahimili ukame mkubwa kuwahi kutokea katika miongo minne katika eneo la kusini. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Madagascar ni kati ya nchi zilizo hatarini zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi na ina moja ya viwango vya juu zaidi vya umaskini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live