Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

15 wauawa kikatili DRC 

Ff3f8964b04451c800b93518368c6a0f 15 wauawa kikatili DRC 

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIA15 wameuawa na wanamgambo katika kijiji cha Bulongo Jimbo wa Kivu Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Imeripotiwa kuwa watu waliobeba silaha yakiwemo mapanga walivamia jana jioni na kuanza kujeruhi wananchi wa Jimbo hilo huku wengine wakikatwa vichwa.

"Raia wasiopungua 15 wameuawa usiku huko Bulongo eneo la Kivu Kaskazini.” Kikundi cha Kivu Security Tracker (KST) kilichapisha kwenye Twitter jana na kuongeza kuwa Kikosi cha Allied Democratic Forces (ADF) ni washukiwa wa tukio hilo.

Kihistoria ADF ni kikundi cha Waislamu wa Uganda ambacho kimekusanyika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu 1995. Imefahamika kuwa sifa yao ni umwagaji damu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz