Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

13 mbaroni kwa ugaidi Rwanda

Rwanda Picbb 13 mbaroni kwa ugaidi Rwanda

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Rwanda limethibitisha kuwakamata watu 13 wanaotuhumiwa kufanya mashambulizi ya kigaidi katika Mjii Mkuu wa Kigali.

Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na vifaa vya kutengeneza mabomu, nyaya, simu pamoja na silaha za kivita.

"Uchunguzi wetu umebaini kuwa mtandao huu wa kigaidi unafanya kazi kwa kushirikiana na kundi la kijihadi la Allied Democratic Force (ADF) la nchini Congo" Imesema ripoti ya Polisi.

Kundi hilo la ADF linatajwa kuhusika katika matukio mengi ya kigaidi katika nchi za Congo na Uganda, na linatajwa kushirikiana na baadhi ya vikundi vya watu katika mataifa hayo kuendesha magenge ya kigaidi na kujitoa muhanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live