Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

10 wajeruhiwa kwenye ajali ya ndege Senegal

Sk577r 10 wajeruhiwa kwenye ajali ya ndege Senegal

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu kumi wamejeruhiwa katika ajali ya Ndege aina ya Boeing 737 iliyotokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Mji Mkuu wa Senegal, Dakar.

Taarifa kutoka Wizara ya Uchukuzi inasema kuwa Ndege hiyo ilipoteza alama wakati ikiwa inapaa ikielekea Bamako nchini Mali.

Ndege hiyo ya kampuni ya Air Senegal ilikuwa na abiria 85, watalii 79 na rubani wawili na wahudumu wanne wa ndege.

Waziri wa Usafiri na Uchukuzi wa Senegal El Malick Ndiaye amefahamisha kuwa majeruhi walikimbizwa hospitali huku pia shughuli katika uwanja huo zikisitishwa kwa muda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live