Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera awafyeka akina Yondan ikiivaa Kagera

28734 Pic+zahera TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesemaatawatumia wachezaji wenye moyo katika mechi za Ligi Kuu ili kuipa ushindi timu yao.

Yanga inashuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuivaa Kagera katika mchzo wa Ligi Kuu.

Hata hivyo, Yanga iko mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa bila baadhi ya nyota wake; Kelvin Yondan. Benno Kakolanya wanaodai malimbikizo ya mishahara yao.

“Uzuri Yanga ina wachezaji wengi, hatutegemei mchezaji mmoja, anayekosekana wapo wa kujaza nafasi zao, hilo sina shaka nalo,” alisema kocha huyo

Mbali na hayo, Yanga leo inayo nafasi kubwa ya kuitimulia vumbi Simba na kuiwashia indiketa Azam FC inayoongoza Ligi Kuu Tanzania Bara, iwapo itaifunga Kagera Sugar katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Yanga ambayo inakabiliwa na ukata kiasi cha baadhi ya wachezaji wake kuweka mgomo baridi, juzi Alhamisi iliishusha Simba hadi nafasi ya tatu baada ya kuishinda Mwadui FC kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Ushindi huo uliiwezesha Yanga iliyocheza mchezo wa 11 kufikisha pointi 29, iwapo itashinda leo itafikisha pointi 32 moja nyuma ya Azam huku ikiwa na mchezo mkononi, ikizidi kuiacha Simba yenye pointi 27 ambayo imeshacheza michezo 12.

Suluhu ya mchezo wa juzi kati ya Simba na Lipuli ndiyo iliyochangia kuipa Yanga mwanya wa kuanza kuwatimulia vumbi watani zao hao.

Zahera alisema kwa maandalizi aliyoyafanya anayo matumaini makubwa ya kupata ushindi katika mchezo wa leo, hasa ikizingatiwa Uwanja wa Kaitaba kwa sasa ni mzuri baada ya kuwekwa nyasi bandia.

Zahera alisema mshambuliaji wake mahiri Ibrahim Ajibu ambaye alikosekana katika mchezo dhidi ya Mwadui leo anaweza kuwepo kwani ameshafanya mazoezi ya kutosha na wenzake.

Kocha huyo alisema wazi kuwa hajali matokeo bali ataendelea kuwatumia wachezaji wake wanaoonyesha nidhamu mazoezini kwani hakuna mchezaji staa katika kikosi chake.

Ajibu aliipa Yanga ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugara kwenye Uwanja wa Kaitaba msimu uliopita, alitoa pasi kwa Obrey Chirwa aliyefunga bao la kwanza kabla ya yeye kufunga bao la pili lililowapa ushindi.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema mchezaji mmoja atakuwa mzawa na watatu watatoka nje ya nchi kati yao akiwa winga na mshambuliaji mmoja atakayeimarisha safu hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz