Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera amvua unahodha Yondani ampa Ajibu

34839 Pic+yondani Tanzania Web Photo

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Mkongo Mwinyi Zahera amemvua unahodha beki wa kati, Kelvin Yondani 'Vidic' kutokana na utovu wa nidhamu. Yondani ambaye mwanzoni mwa msimu huu alitangazwa rasmi kuwa nahodha wa Yanga akibeba mikoba iliyoachwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye pia alikuwa anacheza nafasi ya beki wa kati, amevuliwa wadhifa huo kutokana na kuchelewa mazoezini pamoja na ukimya. "Niliwapa wachezaji siku tano za mapumziko ili siku ya sita waje mazoezini yeye hakutokea, amezima simu na amegoma. Siwezi kumwacha mtu kama yule anayepaswa kuonyesha mfano kwa wengine afanye hayo hivyo nimeamua nimvue unahodha na kuanzia sasa  nahodha ni Ibrahim Ajibu,"alisema Zahera ambaye ni kocha mwenye msimamo na anachokizungumza. Ikumbukwe pia, Zahera alifanya maamuzi ya kumkataa kikosini mwake mlinda mlango, Beno Kakolanya kwa matatizo kama hayo na mpaka sasa hajajiunga na timu.

Chanzo: mwananchi.co.tz