Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera alivyoibeba Yanga Ligi Kuu Bara

61233 Zahera+pic

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ‘Serengeti Boys’Kelvin John amesema hawezi kucheza Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikisajili wachezaji kwa gharama kubwa.

Kelvin ni miongoni mwa nyota 39 walioitwa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ kwa Fainali za Kombe la Afrika, baada ya kucheza kwa kiwango bora.

Akizungumza kwa simu, Kelvin alisema ana ofa nyingi amezipokea kutoka mataifa mbalimbali ambayo hakutaka kuweka wazi na kubainisha kuwa hadi ifikapo Juni atajua ni timu gani atakwenda kucheza.

“Sina maana kwamba soka la Tanzania halina uwezo, hapana nimesema hivyo kutokana na umri wangu nahitaji kucheza timu ambayo ina kituo cha kulea vipaji kitu ambacho kwa timu zetu za ndani hakuna. Hii ndio inaweza ikawa sababu kubwa ya mimi kakataa kucheza soka la ndani kwani nina ndoto ya kufika mbali,”alisema.

Alisema mipango ya kutimka Tanzania kwenda kujaribu soka la kulipwa nje ya nchi itakamilika mara baada ya kumalizika kwa Fainali za Afcon.

Pia alisema ana furaha kujiunga na kambi ya Taifa Stars na kukutana na wachezaji wenye uzoefu katika soka.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz