Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera ajitwisha lawama Yanga ikilazimishwa sare ya bao 1-1

50556 Zahera+pic

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA Yanga, Mwinyi Zahera amesema matokeo ya sare 1-1, dhidi ya Ndanda waliyoyapata katika mechi ya leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara wameyataka wenyewe.

Zahera alisema hata kiwango ambacho alikionesha refa wa mchezo huo Martin Sanya kilikuwa kizuri na hata wale watu ambao wanamlaumu kuwa alifanya makosa katika mchezo huo kwake wala hayakuyaona.

Alisema wachezaji wangu walifanya makosa kipindi cha kwanza ambayo ilikuwa lazima Ndanda waweze kuyatumia na waliweza kufanya hivyo kwa kutumia moja kati ya waliozipata.

"Uwanja pia si mzuri haswa katika eneo la kuchezea nao naweza kusema ulichangia timu yangu kushindwa kucheza vizuri na kushindwa kupata pointi tatu ambazo ndio yalikuwa malengo yetu na tukashindwa kufanya hivyo tukapata matokeo haya," alisema.

"Katika kipindi cha kwanza hatukuwa tunacheza kwa kuchangamka na kushambulia kwa haraka kwani tulikuwa tunacheza na timu ya chini kwenye msimamo jambo ambalo walituzoea na kuja kwetu kutushambulia kwa haraka.

"Timu kama Ndanda ilibidi tuwape presha kama tulivyofanya katika kipindi cha pili ili wafanye makosa ambayo yangetupa mianya ya kufunga bao zaidi ya moja ambalo tulilipata kipindi cha pili," alisema Zahera.

Yanga walisawazisha bao kipindi cha pili dakika 61, kupitia kiungo Tshishimbi kwav kichwa akipokea krosi ya beki wa kati Kelvin Yondani.



Chanzo: mwananchi.co.tz