Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera afuata pesa zake Yanga

86041 Pic+zahera Zahera afuata pesa zake Yanga

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

ALIYEKUWA kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kesho Jumatano alfajiri anarudi Tanzania kufuata malimbikizo ya madeni yake kwa uongozi wa klabu hiyo.

Zahera alifungashiwa virago vyake baada ya kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo ambapo nafasi yake inakaimiwa na Bonface Mkwasa.

Zahera amesema hakuna mahala aliposaini barua ya kutimuliwa Yanga na hajalipwa malimbikizo ya madai yake hivyo anarudi kufuata.

"Nitafika Tanzania saa 8 alfajili kesho Yanga hawajanilipa fedha yangu na bado sijasaini barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo,".

"Siwezi kuendelea kukaa huku nikiwa bado sijamalizana na Yanga narudi tena Tanzania kwaajili ya kudai fedha zangu na kusaini hiyo barua ya kuvunja mkataba kama wao wanavyotaka," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz