Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera afichua siri ya kipigo DR Congo

63975 Pic+zahera

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Timu ya Taifa DR Congo imeanza kwa kupoteza katika Fainali za Afcon baada ya kukubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa Uganda.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mwinyi Zahera amefichua siri ya kipigo hiko ni kutokana na wachezaji wake kuchoka baada ya kutumia muda mwingi kufanya vipimo.

Zahera alisema baada ya kuwasili Misri, madaktari wa Caf waliwataka wachezaji wao kwenda kufanya vipimo ndipo wachezaji wao wakatumia muda mwingi wakiwa hospitali.

"Tangu saa tano asubuhi wachezaji walikuwa hospital na wa walirudi saa tano usiku hiki ni kitu cha ajabu sana, wachezaji walishindwa hata kuangalia mechi ambayo tupo nayo katika kundi," alisema.

Aliongeza hali hiyo iliwafanya wachezaji wake washindwe kukimbia vizuri kutokana na uchovu waliokuwa nao.

Katika mchezo huo wachezaji wa Uganda walionekana kuutawala mchezo kuliko DR Congo hali ambayo iliwafanya waibuke na ushindi.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz