Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera aanza tambo, awapiga kijembe Msimbazi

34185 Pic+zahera Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Unaweza kusema Yanga wanaupokea mwaka mpya kwa raha huku kocha wake Mwinyi Zahera akianza tambo kwa hasimu wake Simba kwamba huo moto waliouwasha ndio hadi ubingwa.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 50 ikiiacha Azam kwa pointi 10 wakati Simba inayoshika nafasi ya tatu, yenyewe ina pointi 33.

Yanga ilizidi kupaa juzi kwa ushindi wa 16 ilipoichapa Mbeya City mabao 2-1 na ilipata ahueni baada ya Azam kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar.

Simba ilipunguza wigo wa pointi za Yanga kwa kuichapa Singida United mabao 3-0 kabla ya ligi hiyo kusimama kupisha Kombe la Mapinduzi michuano inayoanza kesho Januari Mosi Visiwani Zanzibar.

“Kwanza nilijua kabisa kwamba katika mchezo wetu dhidi ya Mbeya City tutashinda kutokana na wachezaji wangu kuwa na morali ya juu, kwa hapa tulipo hata kama Simba wakisema wacheze mechi zote na kushinda hawawezi kutufikia...bado sana na sisi bado tunahitaji ushindi katika kila mchezo mbele yetu. Hatuachi kitu,” alisema.

Wakati Yanga ikijikita kileleni baada ya kufikisha pointi 50, mshambuliaji wake Herietier Makambo akiwa ndio kinara baada ya kufikisha magoli 11 na kumuacha Eliud Ambokile mwenye magoli tisa.

Azam kwa upande wake, waliokuwa wakiifukuza Yanga, walionja shuri kwa kuchapwa 2-0 na kusalia na pointi zake 40 huku kasi yao ikionekana kuanza kupungua.

Kwa upande wa Simba wao wameendeleza ubabe katika kura viporo vyao baada ya kuifunga 3-0 Singida UTD na kufikisha pointi 33, huku wakiwa na michezo minne mkononi lakini hata wakishinda yote hawataifikia Yanga. Simba ikishinda mechi zote nne za viporo, itafikisha pointi 45.

“Tunapambana, najua hatutafanya makosa, wachezaji wangu wako sawasawa, najivunia na ninamini baada ya mwaka mpya, tutaendelea ushindi. Siwezi kusema ubingwa kwani tuna mechi 38 na mpaka sasa tumecheza mechi 14,” alisema Aussems.



Chanzo: mwananchi.co.tz